1. Timu ya mpira wa miguu
Timu yetu ya Junction ilikuwepo toka
kitambo sana. Miaka ya nyumaa ikiitwa everton squad, enzi zile za kaka zetu
akina Hassan Masoud ‘Pardon’, akina Hassan Msabata ‘bondasi’, akina Peter Njoka
‘Mpita’ Joseph Mbilinyi na Telesphory Mbilinyi‘Tella’, Nassoro Mumba, Mfaume
Mumba ‘mzee wa commonsense’, Juma Mkeso ‘Zagallo’, Kibwana Mangoma, Modestus
Nditi, Bahati Ngatunga, Mzee Shonga, Nathaniel Kipanga, Salum Masoud ‘msauz’,
Kilala, Bakari Mangoma, Mohamed Kazibidii na wengeneo ambao sijakumbuka
kuwataja hapa kwa sasa. Enzi zile uwanja ukiwa nyuma ya ofisi ya CCM. Hawa
jamaa walipiga mpira kuwakilisha kitongoji chetu, iwe gozi iwe chandimu twende
kazi. Big up sana wakubwa.
Na kama inavyoeleweka kuwa soka haliendi
bila ya watu waliopo nje ya uwanja, na kimsingi hawa ndo wanaoibeba timu kwa
kusapoti kwenye kushangilia, kuwatia morari na kuchangia kwa hali na mali ili
timu ionyeshe ushindani. Kwenye kundi hili pia walikuwepo wengi kipindi kile,
akina Omary Mkeso ‘babada’, Jumanne Kipande ‘mosile’, Norasco
Kipanga(marehemu), Jabir Shonga, Nassib Mkeso, Harun Mangoma, Hamis Kahorolela,
Brother Edward Mikao, Ally Ndulli na wengineo. Salute kwenu wakubwa.
Kizazi cha Junction mpya.
Baadaye kukaja kizazi kipya cha timu ya
mpira na kuzaliwa kwa jina la Junction. Hiki ndo kizazi chetu, kuanzia katikati
mwa miaka ya 90. Acha masihara hii timu ilikuwa ya aina yake. Yaani kuanzia
wachezaji, viongozi hadi mashabiki. Kulikuwa na mshikamano na mapenzi ya timu
kiasi kwamba hata mechi tulizopoteza kwa magoli mengi, tulirudi nyumbani tukiwa
na morali na tukiamini mechi ijayo tutafanya vizuri. Kwanza ngoja nijaribu
kukumbuka kikosi cha kwanza kilivyokuwa;
1.
Uledi
2.
Issaya (RIP)
3.
Mode
4.
Charles
5.
Dulla
6.
Issa (mimi)
7.
Rogatus
8.
Silly
9.
Mapa
10.
Juma Kabweza
11.
Amiri.
Wachezaji wengine kama kina Bondasi, Kassim Mkeso, Nuni, Amani Shonga (RIP), Yassin Mumba, Said Masho, Abdalah Mumba, Tufuli, Masoud Kipande, Hassan Kipande ‘diria’ na wengine wengi. Akiwemo mshikaji wetu mmoja aliyekuwa na kipaji cha aina yake Ally Masoud mdogo wake Pardon… jamaa alikuwa noma, sema ndo aliondoka kabla mambo hayajachanganya.

Ubora hasa wa timu ya Junction ya kizazi hiki hadi ikatokea kujulikana
sehemu mbalimbali mjini songea ulitokana na mambo makuu manne;
1) Kikosi kilikuwa na wachezaji watano wenye vipaji vya hali ya juu sana katika kusakata kabumbu. Vijana hawa, kwa kweli kabisa, wangepata nafasi ya kuendelezwa wangali wadogo wangefikia viwango si tu vya Simba na Yanga, bali vya kimataifa kwenye mpira. Issaya (marehemu) – beki wa pembeni, Abdalah Twaib ‘Dulla’ – beki wa kati, Mapambano – kiungo mshambuliaji, Rogatus na Amiri – washambuliaji wa pembeni. Na kocha mchezaji wetu ambaye alikuwa anakuja na kuondoka, Makanyanga.
Ilikuwa vijana hawa wakichanganywa kwenye kikosi na wachezaji wengine wenye viwango vya kawaida kama mimi mwenyewe, tulitisha kwa kweli. Tunapiga mtu magoli alafu tukirudi kitaa Nuni na Tufuli wanaliwasha.

2)
Nje ya uwanja timu ilikuwa na mashabiki
walioisapoti timu kwa namna ya kipekee kabisa, kiasi cha kutufanya sisi tuliokuwa
tunapeperusha bendera ya Junction uwanjani kujituma na kufurahia mchango wa
kila mmoja wetu katika timu. Watu hawa muhimu ni kama Yusuph Mateka, Shabani, Babada, Silaju Mkeso, Seif Mabinya, Mzee
Mtemeke, Kaka yetu Nassib Mkeso, Mosile, Jabir, Mchawa, Mfaume, Tirilo, Mzee
Sokoni, brother Mchebwedee, Edward, Mzee Simba, Habibu, brother Shaban Kipande,
Mtimkavu, Tella, Mzee Kazibidii, Mzee Ngatunga, Juma Mkeso, Mapinduzi Mkeso,
Crodwick Mapunda, Patrick Simba(RIP), Simon Kipanga, Said Pazzy, bila kumsahau
Kabi mzee wa Junction Tulia, na wengine. Hawa walileta mshikamano, kutoa
hamasa, na waliipa timu uzito ikaonekana kweli tupo serious na tunajua
tunachokifanya. Big Up kwenu.
Bila kusahau sapoti ya dada zetu na mama zetu ambao kwa kweli walitutia
moyo na kutufanya tujitume uwanjani ili tuwafurahishe, na mara nyingine ili
watufurahishe (mzee wa commonsense upo hapo?). Hawa ni akina Mama Mtemeke, Mama
Pili(RIP), Mama Filly, Mama James, Mama Michael, Mama Gavana, Mama Sokoni, Mama
Mwang’anga(RIP), Halima Mangoma, Salima Lutumbo, Zaidan Koplo, Stahimili, Zamaradi
Makanyanga(shemeji yetu), Mama Adam, baadhi ya akinadada wa kwa Kipande na wengine wengi ambao walisapoti timu kwa
kuja uwanjani na kwa namna nyingine, BigUp kwenu pia.
3)
Timu ilikuwa na viongozi wabunifu na wenye
kujituma; orodha hii ikiongozwa na mimi mwenyewe, Issa Kanguni, Yusuph Mangoma,
Mzee Mtemeke, Wellnery Njoka, Nuni Amani, Juma Kabweza na wengine.
4)
Timu ilikuwa na mvuto kwa kuwa tulianza tukiwa
tunacheza kama underdogs yaani timu
inayopewa nafasi ndogo sana ya kushinda, lakini tulikuwa tunatoa ushindani wa
hali ya juu sana. Hiyo ilisaidia timu yetu kufahamika na kuwa na mashabiki
mbali. Ikatusaidia pia hata kupewa uwanja wa mazoezi wa kwenye eneo la shule ya
Songea Boys, enzi zile mwalimu wa michezo akiwa mwalim Jimma.
Zipo mechi na matukio kibao ya kukumbuka katika kipindi kile, yote yatakujia kwenye ukurasa huu... kama mkao wa kuhabarika.

0 comments:
Post a Comment