Luhira ni kitongoji kilichopo katika kata ya seed
farm kwenye halmashauri ya Manispaa ya Songea, kilometa nne mashariki kwenye
barabara iendayo Tunduru. Ni eneo lenye umuhimu wa aina yake katika ustawi wa
mji wa Songea kutokana na kuwa na vitu kadhaa, baadhi yake ikiwa ni mito miwili
ya kudumu yenye maji safi wakati wote wa mwaka, mto fataki na mto luhira ambao
kwa sasa ni mto wa hifadhi unaotumika kwa mradi mkubwa wa usambazaji maji. Pia
Luhira kuna shule kongwe ya sekondari ya Songea Boys High School ambayo kwa
kweli ni miongoni mwa taasisi kubwa kabisa za elimu za umma nchini. Pia kuna
mlima Unangwa.
Luhira ni kubwa, na imegawanyika katika mitaa kadhaa, ambayo imepewa majina kulingana koo zilizokuwa zikiishi maeneo hayo tangu zamani.
i.
Kwa Mchawa
ii.
Kwa Mangoma
iii.
Kwa Mkeso
iv.
Kwa Mngwale
v.
Kwa Kipande
vi.
Kwa Msabata
vii.
Kwa Kapolo
viii.
Kwa Koplo
ix. Kwa RupiaJamii ya wanaluhira ni jamii mchanganyiko yenye watu wa makabila tofauti. Mitaa yetu ina majina ya koo si kwa maana ya kuwa eneo hilo linakaliwa na wanaukoo wenye jina hilo pekee, la. Ni kwa sababu hapo zamani eneo fulani lilikuwa likimilikiwa na watu wa ukoo fulani wakiishi na kuendesha shughuli zao nyingine za uzalishaji mali.






Hongera
ReplyDeleteYour post is very informative. Did you know that women can buy Abortion Pills online USA to maintain privacy and safety during difficult times? Keep spreading awareness about accessible healthcare options.
ReplyDeleteGreat insights! Many women face challenges accessing care, which is why websites like abortionpillrx247.com let you buy Abortion pills online with 24/7 support.
ReplyDelete